• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

NFRA

imewekwa Tar: May 11th, 2022

DOLA MILIONI 6 ZAKAMILISHA UJENZI WA VIHENGE VYA KISASA SUMBWANGA

Na. OMM Rukwa

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Sumbawanga imefanikisha ujenzi wa vihenge nane na ghala moja la kisasa vitakavyoongeza uwezo wa kuhifadhi mazao tani 25,000 kwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 6.019.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti aliyetembelea mradi huo uliopo eneo la Kanondo katika Manispaa ya Sumbawanga alisema kukamilika kwake ni mafanikio kwa wakulima wa Rukwa na Taifa kuwa na uwezo wa kuhifadhi nafaka kisasa.

“Mradi huu utakuwa mkombozi kwa Taifa kuhifadhi akiba yake ya chakula kwa njia ya kisasa ambapo wananchi wa Rukwa ndio wanufaika wakubwa kutokana na vihenge hivi kuwa hapa Sumbawanga” alisema Mkirikiti.

Akitoa taarifa ya mradi huo , Mhandisi Mkazi toka kampuni ya M/s Unia Araj  ya Poland Mhandisi Haruna Kalunga alisema mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2020 umehusisha ujenzi wa vihenge nane, majengo 6,ghala moja, mzani mmoja na uzio  kuzunguka eneo hilo.

Mhandisi Kalunga aliongeza kusema vihenge hivyo vya kisasa vikubwa vipo sita na vidogo viwili pamoja na miundombinu yake vina uwezo wa kubeba tani 20,000 ambapo ghala la kuhifadhia mazao limekamika pia likiwa na uwezo wa kubeba tani 5,000  na kuwa mradi huo umekamilika mwezi Machi mwaka huu na majaribio tayari yamefanyika mwezi Aprili mwaka huu.

“Mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa Dola za Kimarekani 5,417,459 sawa na asilimia 90 ya fedha zote za mkataba ambazo ni Dola za Kimarekani 6,019,399” alieleza Mhandisi Kalunga.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kalunga alitoa ombi kwa serikali kupitia VETA kuwarasimisha vijana wa kitanzania wapatao 60 ambao walioshiriki kazi za ujenzi wa vihenge vyote na miundombinu yake kutokana na uwezo na uzoefu wao.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tunaomba vijana wazalendo walioshiriki ujenzi wa mradi huu warasimishwe na VETA kupitia mpango wa urasimishaji ujuzi nje ya mfumo rasmi” alihitimisha taarifa yake Mhandisi Kalunga.

Naye Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga Marwa Range alisema kufuatia kukamilika kwa mradi huo Wakala tayari umeanza kutumia miundombinu hiyo kuhifadhi mazao na kuwa utasaidia kuboresha hali ya uhifadhi nafaka kwa matumizi ya Taifa.

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kupitia mpango wa Storage Capacity Expansion Project (SCEP) ilipokea mkopo wa fedha wenye masharti mepesi toka serikali ya Poland kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa vihenge vya kuhifadhia mazao na miundombinu yake kwenye mkoa wa Rukwa.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA - 2025, KULINGANA NA MATOKEO YALIYOTANGAZWA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) June 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TUME YA UCHAGUZI YAZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA MPIGA KURA KUZINGATIA SHERIA NA MAELEKEZO

    July 31, 2025
  • RUKWA YAENDELEA KUCHUKUA HATUA THABITI KUDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    July 28, 2025
  • RUKWA YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU JUMUISHI YA TAIFA YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

    July 24, 2025
  • INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UCHAGUZI KUZINGATIA VIAPO VYAO NA MAADILI YA KAZI

    July 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa