Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuomba raia wa nchi ya Oman Maher Al Barwan anayefanya ziara ya kulizunguka bara la Afrika kwa pikipiki kuhakikisha anautangaza mkoa wa Rukwa na fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Mkoa.
Amemuambia kuwa Mkoa wa Rukwa una ardhi ya kutosha kwa wawekezaji kuja kuwekeza pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kuimarisha barabara pamoja na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kutapelekea maeneo mengi ya Mkoa kufikika kwa urahisi na wale wanaotoka nje ya mkoa kufika kwa haraka.
“Mji wetu ni mzuri, una amani, Wafipa wakarimu na tunaendelea kuudumisha utamaduni, wakati mwingine unaweza kuona kuna machifu na mambo mengi mazuri,” Alieleza.
Waliongea hayo wakati Albarwani alipotembelea katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kufanya maongezi na mkuu huyo ikiwa ni pamoja na kujitambulisha na kutaka kusikia fursa na vivutio vilivyopo katika Mkoa wa Rukwa na kumuahidi kuwa atautangaza Mkoa wa Rukwa katika msafara wake huo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa