Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, leo Desemba 31, 2024, amekabidhi zawadi za msimu wa Sikukuu za Mwaka Mpya kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum katika mkoa wa Rukwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Mhe. Makongoro Nyerere alimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuwajali watoto yatima na watu wenye mahitaji maalum, akisema kuwa zawadi hizo zimeleta furaha na tabasamu kwa walengwa msimu huu wa sikukuu.
Zawadi zimekadhiwa katika Vituo vya Malezi vya Katandala na Bethania, Gereza la wafungwa la Mollo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za msingi Sandulula, Laela, na Kamnyalile zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa