RAS MCHATTA AKAGUA MIRADI HALMASHAURI (W) SUMBAWANGA
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Rashid Mchatta amefanya ziara ukaguzi wa miradi ya sekta ya afya na elimu inayotekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa kutembelea kata ya Muze na Mtowisa.
Katika ziara hiyo aliyoifanya leo (Januari 25,2023) Mchatta alikagua mradi wa ujenzi wa madarasa mapya katika shule za sekondari Mazoka (vyumba 4) ,shule shikizi ya msingi Mkuyuni, shule ya msingi Mkamanyi, Uzia na shule ya sekondari Vuma ambapo miradi ya madarasa imekamilika na kuagiza yatumike .
Akiwa katika shule shikizi ya Mkuyuni RAS ambapo kuna mradi wa ujenzi wa nyuma ya mwalimu, ameelekeza halmashauri ifanye utaratibu wa kupima eneo na kuweka alama ili kuepusha uvamizi wa maeneo hayo.
Kwa upande wa sekta ya afya , Mchatta amekagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Muze na hospitali ya wilaya Mtowisa kuona mwenendo wa utekelezaji wake.
Akiwa Hospitali ya Mtowisa alielezwa kuwa mradi huo ulianza mwaka 2020/2021 na kuwa hadi sasa umetumia zaidi ya shilingi Bilioni 3.4 lakini bado haijakamilika huku baadhi ya majengo yakiwa hayatumiki .
Mchatta ametoa wito kwa uongozi wa halmashauri kusimamia kwa karibu mradi huo kwa kuhakikisha mkandarasi anatekeleza mkataba ili kazi ikamilike na huduma ziendelee kutolewa kwa wananchi pamoja na kuzingatiwa kwa thamani ya fedha.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa