• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC awaasa wanahabari kutangaza fursa za uwekezaji Mkoani Rukwa

imewekwa Tar: May 4th, 2017

Mkuu wa Moa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen awaasa wanahabari wa Mkoa wa Rukwa kutumia vizuri kalamu zao na visemeo vyao katika kutangaza fursa nyingi za uwekezaji zilizopo katika Mkoa.

Ameyatamka hayo katika maadhimisho ya siku ya habari duniani ambayo huadhimishwa tarehe 3, Mei ya Kila mwaka ambapo kitaifa ilifanyika katika Mkoa wa Mwanza na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo (Mb) Mh. Harrison Mwakyembe.

“Mkoa wetu ni wa Kilimo cha mazao ya chakula, biashara, ufugaji, uvuvi, utalii na madini.   Shughuli ambazo zinahitaji msukumo wa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na ninyi waandishi wa habari kusemea kwa nguvu maeneo hayo,” Mkuu wa Mkoa alifafanua.

Mh. Zelote alisisitiza kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kutangaza fursa zilizopo katika mkoa wa Rukwa na watu wengine walio nje wakaweza kujua fursa hizo na kuungana na wananchi wa Mkoa huu ili kuwekeza hasa viwanda ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa ili kukamata masoko yaliyo ndani, nje ya Mkoa na nchi jirani.

Katika kuhakikisha kuwa wanahabari wanapata habari wanazozipata kwa wakati kutoka katika Taasisi za Kiserikali Mkoani Rukwa Mkuu wa Mkoa aliagiza kuwa Halmashauri zote zihakikishe zinatoa habari bila ya uwakwepa wanahabari pindi wanapozihitaji habari hizo.

 “Sitaki kusikia Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wanakwepa kutoa habari.  Ni vyema sasa Halmashauri zione umuhimu wa kuwatumia wanahabari kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka na nisisitize uwepo uwazi kwa shughuli zote za maendeleo katika Halmashauri zote.” Mkuu wa Mkoa alibainisha.

Pia aliwasisitiza wanahabari pindi waziandikapo habari zao basi wasisahau kuweka mbele umoja wa Taifa letu, usalama wetu, uhuru wa nchi, uadilifu na maadili ya jamii kwa upande mwingine.

Maadhimisho hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Kimkoa yalihudhuriwa na wanachama mbalimbali wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Rukwa (RKPC) pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiwemo wawakilishi wa mashirika na taasisi mbalimbali za seriikali nchini.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa