RC MAKONGORO ATAKA JITIHADA ZAIDI KUONGEZA UFAULU.
Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari kuongeza jitihada Ili kuinua zaidi kiwango cha ufaulu.
Mheshimiwa Makongoro ameyasema hayo leo Januari 31, 2024 wakati wa kikao Cha tathmini tathmini ya shughuli za elimu Mkoani Rukwa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa St. Maurus Chemchem, Sumbawanga.
Mheshimiwa Makongoro amewataka viongozi wote kuanzia ngazi za mitaa hadi Mkoa kwa kushirikiana na walimu na wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula chenye lishe bora mashuleni akieleza kuwa itasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Rukwa amewataka viongozi wote, wazazi na walimu kukomesha utoro kwa wanafunzi kwani utoro unachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufeli.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewapongeza walimu na wadau wote wa Elimu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuinua kiwango cha taaluma Mkoani Rukwa
.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa