Na Khadija Dalasia - Kalambo
Leo Julai 15, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Forodha cha Kasesya kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Wilayani Kalambo.
Katika ziara hiyo, amepokea taarifa ya mafanikio makubwa ya kituo hicho ikiwemo ongezeko la makusanyo kutoka milioni 800 kwa mwezi Mwaka 2022 hadi bilioni 3 kwa mwezi kwa Mwaka 2025
RC Makongoro amesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha miundombinu ya Kasesya 2025/2026 na kukifanya lango kuu la biashara na maendeleo kwa Rukwa.
"Tunataka Kasesya iwe kitovu cha fursa kwa wafanyabiashara na wananchi " amesema Makongoro
Amesihi wawekezaji kuwekeza katika maeneo ya huduma kama maegesho ya malori, hoteli, afya, elimu na huduma kwa wasafiri.
RC Makongoro amekagua pia miradi ya elimu, afya na daraja katika Wilaya ya Kalambo, akisisitiza usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa miradi
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa