Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa utekelezaji bora wa majukumu yao, ukiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa viwango stahiki na ndani ya muda uliopangwa.
Akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga leo Julai 22, 2025 Mheshimiwa Makongoro ameeleza kuridhishwa kwake na mafanikio yaliyopatikana ikiwemo kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa miaka tisa mfululizo, na ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 125 ya lengo la ukusanyaji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
“Manispaa ya Sumbawanga imeendelea kuwa mfano wa kuigwa kutokana na weledi na uwajibikaji wa watumishi wake. Nawaomba muendelee kushirikiana kwa karibu katika kuwaletea wananchi maendeleo yanayoonekana,” alisema.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya kusikiliza kero na changamoto za watumishi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa