Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere amewataka wahitimu wa Astashahada ya Elimu Msingi na Elimu Awali kutoka Chuo cha Ualimu Sumbawanga kutumia elimu na maarifa waliyoyapata kuchangia mabadiliko katika sekta ya elimu nchini.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameyasema hayo leo Mei 02, 2024 alipokuwa akiwatunukia vyeti wahitimu hao katika mahafali ya 30 ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga.
Mheshimiwa Makongoro amewasihi kuitumia elimu waliyoipata kufanya kazi ya ualimu kwa kuzingatia weledi, sheria, miongozo na maadili ya kazi ya ualimu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa