Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amempongeza Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu.
Pongezi hizo amezitoa leo asubuhi kabla ya kufungua mafunzo ya utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) kwa watoa huduma za afya mkoani rukwa,yenye kusisitiza tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
“Jambo la kwanza Ndugu Tixon Nzunda nikupe hongera sana, hongera kweli kweli, nina ila sababu ya kukupongeza kwasababu ni asubuhi ya leo tumeamka na haya mapya kwamba wewe siyo Katibu Tawala tena ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, hii tunasema kwamba Rukwa inaingia kwenye nafasi nzuri ya kutoa watendaji waadilifu, wachapakazi, wapenda ushirikiano, kujituma, Maadili, hongera sana,” Mh. Zelote alisisitiza.
Uteuzi huo ambao umefanyika alfajiri ya leo umebainisha kuwa Ndugu Bernard Makali ndiye atakayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Tixon Nzunda.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa