Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa Shilingi 150,000/= kwa vikundi vitatu vya muziki ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na vikundi hivyo katika kukuza utamaduni na sanaa ya mtanzania.
“Kila kikundi kilichokuja hapa, vile vitatu navipa shilingi 50,000/=, na hii ni chachu tu kwa makundi mengine, waweze kuona uzito wa kutunza na kuimarisha tamaduni zetu lazima tuendeleze tamaduni zetu, taifa lisilokuwa na utamaduni limelala, na sawa na kufa kabisa,” Alisema.
Aidha, aliwataka vijana kujishughulisha na sanaa za utamaduni ili kulinda na kuenzi na kutopoteza nembo ya taifa na utambulisho kama watanzania na kasha kutumia nafasi hiyo kivipongeza vikundi vitatu; kikundi cha Kwaya ya Sopa, kikundi cha ngoma za utamaduni cha maporomoko na kikundi cha muziki wa kisasa cha Wasafi boys.
Alitoa zawadi hiyo katika maadhimisho ya siku ya utundikaji mizinga kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kijiji cha kisumba, kata ya kisumba, Wilayani Kalambo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa