Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati ya ushauri ya maendeleo ya wilaya (DCC) kabla ya kufanya kikao cha kamati ya ushauri ya maendeleo ya mkoa.
Amesema kuwa kwa muda mrefu wakuu wa wilaya wamekuwa wakisubiri kikao cha RCC bila ya kuwa na taarifa kamili ya vikao vya DCC kwakuwa hawavitekelezi kama inavyotakiwa.
“Vikao hivi vipo kisheria na ni mara mbili tu kwa mwaka, sasa kila siku tunakutana ngazi ya Mkoa tu na kujadili mambo ya mkoa bila ya kujua yaliyojiri katika ngazi ya wilaya na sioni kama ni muafaka kuendelea na utaratibu huu, hivyo maagizo yangu ni kwamba kabla ya kikao hiki nataka kupata mrejesho wa vikao vya DCC ndipo tuendelee na kikao hiki,”Alisema
Mh. Zelote alisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo ndipo ngazi ya mkoa itaelewa eneo ambalo ngazi ya wilaya imeshindwa kulitekeleza kwa ufanisi na kuhitaji msaada kutoka katika ngazi ya mkoa ili kwa pamoja kuweza kusaidiana namna ya kutatua matatizo hayo na hatimaye kufikisha hudmua bora kwa wananchi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa