• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Rukwa pamoja na Wakuu wa mikoa 10 watoa tamko la kumpongeza Mh. Dk. John Pombe Magufuli

imewekwa Tar: June 26th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameungana na Wakuu wa mikoa 10 kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa, nzuri na ya kizalendo anayoendelea kuifanya ya kutetea na kulinda rasilimali za nchi kwa masilahi ya Watanzania.

Wakuu hao ni kutoka mikoa ya  Singida, Rukwa, Katavi, Kagera, Tabora,Dodoma, Manyara, Geita, Shinyanga, Mwanza na Kigoma.

Wametoa tamko hilo   jana Ijumaa ( Juni 23) kwenye mkutano wa kawaida wa ujirani mwema katika mikoa hiyo ambao  ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.

Mwenyekiti wa mkutano huo, alikuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry.

“Sisi wasaidizi wake (Rais Magufuli) tutaendelea kutekeleza na kuzingatia maelekezo katika utendaji wetu wa kila siku.

Aidha, wakati wote tutakuwa pamoja na wananchi na kuwatumikia kwa kutimiza wajibu wetu kwa uaminifu, uadilifu na tutahakikisha masilahi ya wananchi na Taifa yanapewa kipaumbele cha kwanza,” limesema tamko hilo.

Pia, wakuu hao wa mikoa wametoa wito kwa wananchi na wawekezaji halali wa ndani na nje ya nchi, wamuunge mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi na wakati wote wazingatie sheria za nchi.

“Tutumie fursa nyingi zinazoendelea kutengenezwa kwa hatua hizo za kizalendo anazochukua mheshimiwa wetu Rais Magufuli.  Kwa mafanikio, maendeleo na tija kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda,” limeongeza tamko hilo.

Mkutano huo wa aina yake kufanyika mjini hapa umesisitiza kwamba kuna haja ya kumtia moyo Rais Magufuli ili aendelee na ujasiri wake huo wa kulinda rasilimali za nchi.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa mkutano huo, Mwanry amesema pamoja na mambo mengine wametumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu na wamekubaliana kupeana taarifa mbalimbali za kimaendeleo.

 “Tumekutana hapa kwa mapenzi ya nchi yetu na ya Rais wetu Magufuli. Tuliokutana leo hii, changamoto za mikoa yetu zinafanana. Changamoto hizi ni pamoja na uharibifu wa mazingira, uhaba wa mvua, kilimo cha kuhama hama na uhamiaji haramu,” amesema Mwanry na kuongeza;

“Kwa hiyo tukiacha kila mkoa utatue changamoto hizi kivyake, hatutafanikiwa kizitatua.Tumekubaliana kukutana mara kwa mara ili changamoto zinazotukabili sote tuzipatie ufumbuzi wa kudumu kwa pamoja.”





Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa