• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Sendiga Akutana na Wazee

imewekwa Tar: September 12th, 2022

RC SENDIGA AKUTANA NA WAZEE WA RUKWA, AOMBA USHIRIKIANO

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amewaomba wazee na viongozi wa madhehebu ya dini kuunga mkono jitihada za Serikali kusukuma agenda za maendeleo ili mkoa upige hatua za kiuchumi.

Sendiga amewasihi wazee hao kuliombea taifa na viongozi wake ili mipango inayowekwa izingatie maslahi mapana ya taifa na kujibu changamoto za maendeleo ya Rukwa hatua itakayowezesha ustawi wa jamii.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo leo (12.09.2022) mjini Sumbawanga wakati wa kikao na wazee pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini toka katika wilaya zote tatu za mkoa wa Rukwa akiwa na lengo la kujitambulisha kwao na kuwaelezea mipango inayotekelezwa na Serikali.

“Nawaomba msaidie kuombea nchi yetu, tumwombee pia Rais wetu Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuiongoza nchi yetu vema katika kujiletea maendeleo kwani malengo yake ni mizuri”, alisema Sendiga.

Katika kikao hicho Sendiga aliwaeleza wazee kuwa wanalo jukumu la kusaidia na kushauri viongozi na watendaji wa Serikali ili shughuli za maendeleo za mkoa wa Rukwa ziwe kwa ubora hatua itakayoondoa changamoto kwa wananchi.

Nao wazee kwa nyakati tofauti akiwemo Honarama Mwimanza mkoani wa Sumbawanga alimkaribisha mkuu huyo kwenye mkoa wa Rukwa na kumsihi afuate nyendo za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia shughuli za maendeleo ya watu.

Kuhusu utekelezaji wa miradi , Meda Chipamba Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Mazwi aliomba uongozi wa mkoa uwe na usimamizi wa karibu wa watendaji na wakandarasi wa miradi ili ikamilike kwani wananchi wengi wanakerwa na miradi mingi kutoisha.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Sendiga ametoa miezi miwili kwa Katibu Tawala Mkoa huo Rashid Mchatta kukaa pamoja na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanamaliza tatizo la uwepo wa maboma ya shule yasiyokamilika na kupelekea watoto kukaa chini.

Sendiga ameyasema hayo leo wakati akizindua miongozo ya kuboresha elimu na kuongeza “Natamani kuona sekta ya elimu ikipiga hatua, usisikie raha kuona mkoa wetu uko nyuma kielimu” alisema Sendiga.

Mwisho.

Matangazo

  • HOTUBA YA BAJETI YA TAMISEMI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 May 05, 2023
  • Bei ya Mbolea za Rukuzu kwa Wakulima August 31, 2022
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi April 20, 2022
  • Hotuba ya Bajeti ya WN -OR TAMISEMI 2022/23 April 20, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAZAZI WAPATIENI WATOTO ELIMU KUHUSU HEDHI SALAMA

    June 02, 2023
  • WAWEKEZAJI KUTOKA ZAMBIA WAVUTIWA NA BANDARI MKOANI RUKWA

    May 28, 2023
  • MRADI WA MAJI WAZINDULIWA KISA

    May 15, 2023
  • ZAHANATI YA MPONA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA YAZINDULIWA

    May 15, 2023
  • Angalia Zote

Video

Serikali Kuimarisha mahusiano na Sekta Binafsi
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0739862632

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa