Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwenda kujifunza namna bora ya kurasimisha makazi yao kwa kushirikiana na halmashauri kwa wananchi wa mtaa wa Sokolo katika kata ya Kizwite, Manispaa ya Sumbwanga.
Pamoja na kusifu jitihada hizo za wakazi hao pia ameitaka manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanakuwa karibu na wakazi hao ili kuwa na taarifa zilizosawa kwa pande zote kuliko kuwa na sintofahamu ya michango inayochangwa na wananchi pamoja na huduma inayotolewa na Manispaa kwa wananchi hao na kuwataka wananchi hao kutoa michango kama walivyokubaliana.
“Niwatake wananchi wenyewe, niwaombe mchangie kama vile ambavyo mmekubaliana, gharama hizi za kuchangia kiwanja 120,000/= sio kubwa ni ndogo, mahala pengine wanagawiwa viwanja kwa mita za mraba na mita moja ya mraba inakwenda mpaka shilingi 3000/= amabzo ni nyingi kwasababu kiwanja kimoja kinaweka kuwa na mita za mraba labda 600 ukizidisha na shilingi 3000/= unapata zaidi ya hiyo 120,000/= lakini hapa kwa pesa hiyo unapata mpaka hati miliki hili ni jambo la kulichangamkia,”
Mradi huo wa urasimishaji makazi ulianza mwaka 2016 kwa makubaliano ya wakazi wa mtaa wa Sokolo na Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mtaa una jumla ya viwanja 853 na kaya 350 huku kila kaya ikitakiwa kulipia Tsh. 120,000/= huku Shilingi 9,204,000 zikiwa zimekusanywa kwa baadhi ya kaya ambapo jumla ya gharama za mradi ni shilingi Milioni 30.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa