Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuanzisha mchakato wa kinidhamu na uchunguzi mara moja dhidi ya Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wialaya ya Kalambo kutokana na utendaji kazi wake usioriddhisha..
Amesema kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akichelewesha juhudi za serikali baada ya kushindwa kumaliza ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mwimbi kwa wakati na kuchelewa kuanza ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Legeza mwendo hata baada ya kupatiwa Shilingi Bilioni 1.1 na serikali kwaajili ya vituo vyote viwili vilivyopo katika halmashauri hiyo.
“Huyu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo utendaji wake siridhwi nao hata kidogo katika mazingira ya sekta ya afya kwa ujumla wake, ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika kituo cha afya cha Mwimbi ulianza mwezi wa nane mwaka 2017 mpaka leo naongea hapa mwezi wa tano mwaka 2018 kituo cha afya kile bado hakijakamilika,” Alisema
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wauguzi katika siku yao ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika kata ya Laela, Wilaya ya Sumbawanga.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa