Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembela ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) na kutokuta hata mfuko mmoja wa mbolea huku wakulima wakijiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mh. Wangabo amefanya ziara fupi katika maghala kadhaa ya wafanyabiashara binafsi pamoja na makampuni yaliyopo mjini sumbawanga na kukuta shughuli za uletaji wa mbolea ukiendelea kwa maandalizi yam simu wa kilimo huku Kampuni ya Mboleaa Tanzania (TFC) ikikosa hata mfuko mmoja katika ghala lao jambo lililowashanga walioambatana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.
“Tutawasiliana na viongozi wa TFC ili tuweze kujua kwanini hawaleti mbolea ya kutosha wakati hii ni kampuni ya serikali inaweza ikaleta mbolea nyingi kuliko hata hao wengine lakini badala yake “godown” (ghala) kubwa lakini hakuna kitu, nini manufaa ya TFC sasa,” Alihoji.
Awali akisoma taarifa ya kampuni hiyo msimamizi wa ghala hilo Jelio Mahenge alisema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 207/2018 kampuni ilifanikiwa kusambaza tani 1082 na kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kampuni imejipanga kuleta jumla ya tani 2500 kwa awamu ya kwanza.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kampuni inafanya jitihada zote za hali na mali kuhakikisha uletaji wa mbolea unatekelezeka ndani ya mwezi huu wa kumi na moja ili kuendana na msimu wa kilimo na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla,”
Msimu wa Kilimo wa mwaka 2017/2018 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 24,000 za Mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 mkoa unatarajiwa kutumia zaidi ya tani 34,000 na mpaka mwanzoni mwa mwezi huu Mkoa umepokea tani 363.75 ambazo tayari zikiwa ndani ya maghala ya wafanyabiashara wa mbolea na nyingine zikiwa njiani.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa