• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo aililia MV Lyemba kuhudumia wananchi ziwa Tanganyika

imewekwa Tar: February 9th, 2020

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameishauri Mamlaka ya Bandari nchini kuona umuhimu wa kuifufua MV Lyemba ambayo ilikuwa ikitoa huduma ya kubeba mizigo na abiria katika ziwa Tanganyika ambapo kwa sasa hakuna hata meli moja inayotoa huduma ya kubeba abiria katika ziwa hilo linalounganisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma na nchi za jirani ikiwemo Zambia pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya watu wa Congo.

Mh. Wangabo amesema kuwa hali ya usafiri katika ziwa tangayika sio nzuri ni mbaya kutokana na wananchi kupanda majahazi, mitumbwi na bodi ambapo mara kadhaa wamekuwa wakijazana jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Maisha ya wananchi hao.

“Hili jambo hili Mamlaka ya Bandari pamoja na vyombo vuingine vinavyohusika mfanye haraka sana kwakweli ile meli ya MV Lyemba kwakweli ni mkombozi katika hili ziwa Tanganyika kwasababu hakuna chombo kingine kikubwa mbacho kinaweza kikasaidia hawa wananchi pamoja na mizigo yao watu wanahangaika sana na ni miaka sasa imekuwa ni muda mrefu, miaka kadhaa imekwishapita kwahiyo hili mlipaswa mlione hata kwa jicho la huruma basi,” Alisema

Na kuonya kuwa isifike hatua watu wakapoteza Maisha kwenye Ziwa Tanganyika ndipo ije kuonekana kuna umuhimu wa kuokoa Maisha ya watu wakati wamekwishaangamia na kuwataka wachukulie jambo hilo kwa uzito mkubwa kabla ya kupoteza maisha ya watu wanaoishi katika mwambao wa ziwa hilo.

Mh.Wangabo ameyasema hayo alipofanya ziara katika Tarafa ya Kasanga kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa km 107 kutoka Sumbawanga – Matai – Kasanga ambapo imekamilika kwa asilimia 97 pamoja na bandari ya Kasanga ambayo imekamilika kwa asilimia 50 akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama ya mkoa pamoja na wataalamu kutoka Mamlaka ya Bandari pamoja na Wakala wa wa Barabara nchini.

Aidha, akitoa taarifa kwa niaba ya Meneja wa Badari hizo za Ziwa Tanganyika Yudas Suwanyi alisema kuwa kuna meli kadhaa zinazohudumu katika ziwa hilo ambazo hubeba mizigo peke yake ikiwemo meli ya MV malagalasi inayomilikiwa na Mtanzania inayofanya safari zake kutegemeana na upatikanaji wa mizigo katika mikoa hiyo.

Wakati akitoa taarifa ya uboreshaji wa bandari hiyo ya Kasanga kaimu mhandisi wa bandari za ziwa Tanganyika Nyakato Lwamnana amesema kuwa pamoja na maboresho ya majengo kadhaa ikiwemo nyumba za watumishi, jengo la kusubiria abiria, maghala, ofisi kadhaa pia kuna upanuzi wa gati unafanyika ambapo kwa sasa kuna gati la urefu wa mita 20 lenye uwezo wa kupokea meli moja na kupanuliwa hadi kuwa na urefu wa mita 120 na kuweza kuchukua meli mbili kwa wakati mmoja ili kuepuka changamoto ya kusubiriana.

“Gharama za mradi ni 4,000,764,000/=, ambapo ulianza tarehe 29.4.2019 mradi ni wa mwaka mmoja mpaka tarehe 28.4.2020 tunategemea mradi huu kukamilika kwasasa umefikia asilimia 50 na muda ambao umekwishapita ni asilimia 76 kama mnavyoona muda mrefu umepita kuliko utekelezaji utekelezaji tuko asilimia 50,” Alisema.

Kwa upande wake meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) mkoani Rukwa Mhandisi Masuka Mkina alisema kuwa imebaki changamoto ndogo ya kupotomoka kwa udongo (landaslide) ili kuweza kukamilisha barabara hiyo iliyoanza kujengwa tarehe 13.1.2010 ambapo hadi kufikia tarehe 31.12.2019 ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 97 na kwa bajeti ya mwaka 2019/2020 serikali imetenga shilingi bilioni 5.8 kumalizia ujenzi huo unaotarajiwa kumalizika mwezi June, 2020.

“Wanampango wa kumleta mtaalamu kusudi aweze kufanya upembuzi wa eneo hili halafu awape muongozo wa nini kifanyike, namna ya kujenga eneo hili ambalo udongo umeporomoka, wamesema wameshampata Kampuni ya Noro Plan Tanzania ndio mshauri ambae atakuja kufanya utafiti hapa kujua chanzo na nini cha kufanya,” Alieleza.

Katika ziara hiyo Mh. Wangabo na timu yake pamoja Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Ndg. Enos Budodi waliridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kuwataka wananchi kutumia fursa zinazopatika kutokana na kukamilika kwa miradi hiyo ya kimkakati ya mkoa.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI October 24, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA - MAPOKEZI YA FEDHA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 3.8 KWA AJILI YA SEKTA YA AFYA October 05, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI- RUKWA September 27, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 13, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • UMOJA NA MSHIKAMANO SILAHA ZA MAFANIKIO MIAKA 62 YA UHURU

    December 09, 2023
  • MAKONGORO AWATAKA WADAU KUILIPA TEMESA KWA WAKATI

    November 21, 2023
  • MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA; WANAFUNZI RUKWA KUGAWIWA VYANDARUA

    October 19, 2023
  • MAKONGORO ATAKA MIRADI IKAMILIKE KABLA YA OKTOBA 30, 2023.

    October 18, 2023
  • Angalia Zote

Video

Serikali Kuimarisha mahusiano na Sekta Binafsi
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0735019734

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa