• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo asaidia nguvu za wananchi katika utekelezaji wa mwaka wa mtoto Rukwa.

imewekwa Tar: June 1st, 2020

Katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya kusoma bila ya kutembea umbali mrefu ili kufika shuleni, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembelea shule za msingi shikizi katika vijiji vya Majengo na Lyazumbi, Wilayani Nkasi ili kuendelea kuhamasisha umaliziaji wa shule hizo ili zisajiliwe na kuweza kufundisha wanafunzi wa kuanzia darasa la nne na kuendelea.

Shule hizo ambazo hivi sasa ujenzi wake umefikia katika hatua tofauti katika ukamilishaji umempelekea Mkuu wa mkoa huo kutoa miezi mitatu ili shule hizo ziweze kukamilika na kusajiliwa ili ziwe shule rasmi na hatimae kupunguza idadi ya vijiji visivyokuwa na shule za msingi kutoka vijiji 59 na kuwa vijiji 57.

Aidha, katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati amewaagiza watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanazifikia kaya zote na kila mdau wa maendeleo katika vijiji pamajona na kata ili kuweza kuchangia ujenzi huo huku Mh. Wangabo akitoa mifuko ya saruji 100 kwa shule hizo ikiwa ni kuunga juhudi za wananchi katika kumkomboa mtoto na shida za kutembea umbali mrefu.

“Mwanzoni mwa mwaka huu tulizindua kampeni ya kuhakikisha kwamba, tunamlinda mtoto, tunathamini haki za mtoto, na ninyi hapa mmetekeleza kwa vitendo, huyu mtoto ana manyanyaso mengi sana, hapa mmesema anatembea km 12 mpaka 15, huu ni unyanyasaji wa mtoto unaofanywa na wazazi wenyewe, na wengine hawaoni kwamba huyu mtoto anateseka, na mateso haya anayatoa mzazi,haoni nasema tu nenda, anamuachia kama kuku anavyoachiwa asubuhi na jioni anafunguliwa aingie,” Alisema.

Wakitoa taarifa katika nyakati tofauti mtendaji wa Kata ya Majengo na Mtendaji Kijiji cha Lyazumbi walisema kuwa lengo la wananchi hao ni kuendeleza ujenzi wa shule hizo ni kuhakikisha Watoto hawatembei umbali mrefu kwenda shuleni na pia kupunguza msongamano katika shule za vijiji vya jirani.

Wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa shule ya msingi Majengo iliyopo, Kijiji cha Majengo, Mtendaji wa kata ya Majengo Nuru Mtoro alisema kuwa wanafunzi hutembea umbali wa Km 12 kwenda na kurudi na hivyo mkuu wa Wilaya alishauri  kuanzisha madarasa matatu kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na mradi wa EP4R mwaka 2018.

”Hii shule ilianza na wananfunzi 120 tu, mpaka sasa tuna jumla ya wanafunzi 457, ambao ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la nne, ambapo kutokana na ongezeko la wanafunzi, mkuu wa wilaya akashauri tuongeze madarasa kutokana na Watoto kubanana na  kukosa jengo la utawala na hatuna nyumba ya mwalimu katika hili eneo, hali inayopelekea walimu kufanya shughuli zao chini ya miti na kipindi cha masika kujibanza kwenye ukuta,” Alieleza.

Naye Mtendaji wa Kijiji cha Lyazumbi Elizabeth Felix alisema kuwa shule ya msingi shikizi ya Kijiji cha Lyazumbi ilianzishwa mwaka 2016 kwa nguvu za wananchi waliolenga kuwaepusha Watoto kutembea umbali wa Km 12 kwenda na kurudi katika Kijiji cha jirani cha Paramawe ilipo shule mama na makao makuu ya kata ya Paramawe, Wilayani Nkasi.

“Shule Shikizi ya Lyazumbi ina madarasa manne, matatu yamekamilika, moja limepauliwa bado kuwekewa sakafu na ujenzi wa umaliziaji wa magebo, shule Shikizi ya Lyazumbi inajumla ya wanafunzi 412, waviulana 118 na wasichana 260 ambao ni darasa la kwanza hadi darasa la tatu, na wanafunzi wa darasa la awali 44, ambao wasichana ni 22 na wavulana 22,” Alisema.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa