• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania PMO - Regional Administration and Local Government Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
      • KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
      • KITENGO CHA MAENDELEO YA JAMII
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo asisitiza wajawazito kujitokeza vituo vya afya kupata huduma bure.

imewekwa Tar: January 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewasisitiza wakinamama wajawazito kujitokeza kupata huduma za kiafya katika vituo mbalimbali vya afya Mkoani humo ili kujiepusha na madhara yanayojitokeza wakati wa kujifungua na kuwaasa kuachana na tamaduni za kujifungulia nyumbani kwani huduma zao ni bure.

Amesema kuwa sera ya afya ya mwaka 2007 inaelekeza kuwa makundi maalum wakiwemo wazee, walemavu, wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanapata huduma za kiafya bila ya malipo hivyo kuwataka watumishi katika vituo vya afya kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kutolewa bure.

Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vitanda 55 ambavyo kati ya hivyo vitanda 20 ni vya kujifungulia na vitanda 35 vya kulalia wagonjwa vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 47, vilivyotolewa na Shirka lisilo la kiserikali Association of Rear Blood Donors (ARDB), na vimetawanywa katika vituo vya afya 9, Zahanati moja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.

“Nitoe wito kwa kina mama wote mnaotoka maeneo jirani na vituo vilivyotajwa, wanaofikia muda wa kuanza Kliniki au wanaofikia muda wa kuanza kujifungua wajitokeze na kufika katika vituo hivyo na kuachana na utamaduni wa kujifungulia majumbani,” Alisisitiza.

Awali kabla ya Kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dk. Boniface Kasululu alibainisha kuwa mahitaji ya chini vitanda katika vituo vya serikali kwa Mkoa ni 1008 na vilivyopo ni vitanda 564 ambavyo ni sawa na asilimia 56 na kisha kueleza sababu za upungufu huo.

“Upungufu huu unachangiwa na ufinyu wa majengo ya kutolea huduma, kwamba eneo ni dogo kiasi kwamba unakosa nafasi ya kuweka vitanda hivyo, lakini kwa msaada wa serikali kuvipa fedha vituo vitano vya afya mkoani kwetu kwaajili ya upanuzi na kuwezesha kupanua huduma hizi tunawaomba wadau wengine waweze kujitokeza kutupa ushirikiano na kuweza kuweka vuitanda vya kutosha katika vituo hivyo,” Alieleza.

Wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, mratibu wa mradi wa ARBD Samwel Mwangi amesema kuwa shirikia hilo linawakilisha makundi ya damu ambayo ni A Negative, B Negative, AB Negative na O Negative leney wanachama 93 ndani ya Mkoa wa Rukwa wenye makundi ya damu mabyo hayapatikani kwa urahisi.

“ili kusaidiana na kutoa huduma kwa wananchi wake ARBD pamoja na shughuli nyinen ni kuhamasisha jamii kujitolea damu na kuhamasisha kinamama wajawazito kuhudhuria Kliniki kwa muda muafaka na kuwahamasisha kinamama hawa kuwapeleka watoto wao kuanza chanjo mpaka wanapomaliza chanjo” Alimalizia.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2026 December 06, 2025
  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI 2025 November 05, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA RUKWA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE

    December 17, 2025
  • BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA SUMBAWANGA YAZINDULIWA, YAAGIZWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MENEJIMENTI KUBORESHA HUDUMA.

    November 28, 2025
  • PPRA YAANZA MAFUNZO KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM KUSHIRIKI UNUNUZI WA UMMA

    December 25, 2025
  • RC MAKONGORO AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA AMANI RUKWA , ASISITIZA UOMJA NA KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YA MKOA

    November 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa