Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameteua timu ya watu watatu kutoka katika madhehebu matatu ya kidini mkoani humo ili kufanya maandalizi na uratibu wa uanzishwaji wa kamati ya amani inayotarajiwa kuanza kazi yake mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu.
Amesema kuwa amani umoja, amani, mshikamano na udugu hauwezi kuwepo ikiwa amani itatoweka, hivyo hakuna budi kuwepo na kamati hiyo itakayoshirikisha viongozi wa dini kutoka pande zote ili kusaidiana katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kufaidi matunda ya amani katika Mkoa nan chi kwa ujumla.
“Na ili tuwe na kamati hii ya amani ni lazima tufanye maandalizi, na haya maandalizi ni lazima yafanyike kwanza na timu ndogo, nimetua timu ndogo ya watu watatu kutoka kwenye madhehebu matatu tofauti ili wafanye maadalizi, wafanye kuratibishwa uanzishwaji wa hii kamati ya amani ambayo ndani ya mwezi mmoja watakuwa wamemaliza shughuli hii, na kuelekea mwishoni mwa mwezi wa saba tutaanza kiako chetu cha kwanza,” Alisema.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano na benki ya CRDB tawi la Sumbawanga iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ikiwajumuisha waislamu wa Mkoa wa Rukwa pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, viongozi wa chama, pamoja na watumishi wa umma.
Akitoa neon la shukurani Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaji Rashid Akilimali alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa maandalizi mazuri ya futari lakini pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza kwa maamuzi ya kuanzisha kamati ya amani katika mkoa ili kuweza kuendeleza mshikamano katika mkoa na kubaki na amani katika mkoa nan chi kwa ujumla.
“Wenzetu wa Syria leo hawajafunga vizuri, wenzetu wa Yemen hawajafunga vizuri, wenzetu kwenye nchi mablimbali hawajafunga vizuri, leo sisi tunafunga sisi kwa amani tumekutana kwenye viwanja hivi, tunafturu vizuri hapa na ‘inshaAllah’ tukitoka hapa tunaelekea kwenye kwenye misikiti yetu kwa amani bila ya kusikia mtutu wa la bughudha, hivi ndivyo tulivyolelewa,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Meneja wa CRDB tawi la Sumbawanga Cornelius Msigwa ameishukuru ofisi ya Mkuu wa mkoa pamoja na uongozi wa BAKWATA Mkoa wa Rukwa kwa kuonyesha mshikamano katika mwezi huu wa ramadhani pamoja na kuendelea kuomba kudumu kwa amani katika mkoa nan chi kwa ujumla.
Walioteuliwa ni Ustadh Mohammed Adam Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Rukwa, ambaye pia ni mwenyekiti wa timu hiyo ndogo. Padre Edgar Mbegu Katibu wa Askofu kanisa Katoliki jimbo la Sumbawanga na Mchungaji Emanuel Sikazwe katibu Mkuu wa Kanisa la Monrovian Jimbo la Rukwa
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa