Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Palela Msongera kuhakikisha anakamilisha ujezi wa hospitali ya wilaya hiyo ndani ya siku kumi na kusisitiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wakandarasi ambao wataenda kinyume na matakwa ya mkataba.
Ujezi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo ulianza mwezi March 2019 na huku mkataba wake ukiwa ni miezi mitatu na ukijumuisha ujenzi wa majengo saba na kugharimu kiasi cha shilingi bilion1.8
Katika kuhakikisha ujezi huo unakamilika kwa wakati mkuu wa mkoa huo Mh.Joachim Wangabo analazimika kukagua maendeleo ya ujezi wa hospitali hiyo kwa kuuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha ujezi huo unakamilika ndani ya siku kumi.
“Kumepoa kabisa na nimepata taarifa kwamba hawa mafundi kuwa kazi haziendi na hakuna hata msumari, watu wamekaa tu siku zinakwenda bado siku kumi, huli ni tatizo la usimamizi, tatizo la halmashauri, tatizo la viongozi kila kitu kilikuwa kwenye mpango, leo wananiambia “Cement” hakuna sijui nini, hizi ni sababu ambazo hazina mashiko, tutafikishana mbali Mkurugenzi ukae ukijua pamoja na viongozi wako wengine wote katika wilaya hii ya Kalambo, huu ni uzembe wa Makusudi wala sio vinginevyo na haipo katika mioyo wenu kwamba kila kukicha mimi nalifikiria jengo, mimi nashindwa kulala usingizi Sumbawanga kule nawafikiria ninyi huku lakini ninyi wenyewe mnalala?
Mkurugenzi mtendaji wa halamshauri hiyo Palela Msongera,amesema tayari wameanza jitihada za kusambaza maji kwenye maeneo hayo na kusema licha ya hilo wameagiza vifaa vya ujenzi ambavyo muda wowote vitafika eneo la ujenzi.
Hata hivyo ujezi wa hospitali hiyo upo katika hatua ya upauaji hivyo endapo ukikamilika kwa wakati itasaidia wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma za matibabu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa