Hatimaye Mkuu wamkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amengilia kati mgogoro wa ujenzi wa kituo cha afya cha Samazi wilayani Kalambo uliodumu kwa zaidi ya miezi miwili baada kutokea kwa mvutano baina ya vijiji vinne huku kila kijiji kikitaka ujenzi ufanyike sehemu yake na hivyo kupelekea uongozi wa halmashauri hiyo kusimamisha harakati za ujenzi huo kwa lengo la kutafuta suluhu.
Kata ya Samazi inapatikana katika mwamabao wa ziwa Tanganyika licha ya hilo kata hiyo imekuwa ikikabiliwa na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa kituo cha afya hali ambayo imekuwa ikiwalazimu wananchi kutembea umbali wa zaidi ya km 20 ili kutafuta huduma za matibabu katika kituo cha afya cha Ngolotwa.
Kwa kuliona hilo serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi million 400 kwa ajili ya ujezi wa kituo cha afya katika maeneo hayo na kutoa maelekezo kwa wananchi kutafuta eneo la ujenzi hali ambayo ilipelekea kila kijiji kutoa mapendekezo yake na huku baadhi yao wakitaka kituo hicho kujengwa juu ya mlima na huku wengine wakiwa na mapendekezo tofauti na kupelekea uongozi wa mkoa huo kuingilia kati suala hilo.
Hata hivyo kabla ya kutoa maamuzi juu ya wapi kituo kijengwe mkuu wa mkoa huo Mh.Joachim Wangabo kwanza akatoa nafasi kwa wananchi kutoa mapenzekezo yao.
Oswald Lwela makazi wa kijiji cha Kisala Alisema kuwa angependa kituo cha afya kujengwa sehemu ya mbele ya kiwanja cha mpira iliyopo juu ya kilima jambo liliungwa mkono na Rosemary Anika mkazi wa Kijiji cha Kipanga Kata ya Samazi.
Baada ya kusilizikiliza maoni ya wananchi Mh. Wangabo alimwagiza mkurugezi mtendaji wa halmashauri hiyo Palela Msongera kuanza ujezi huo mara moja .
“Wote naona mmekubali jipigieni makofi, mimi nimefanya maamuzi, pale ambapo ninyi mmeshindwa kufanya maamuzi mimi nitafanya maamuzi kwa manufaa ya uuma lakini sijafikia huko kwakua mmeshaongea na wataalamu wangu wameshaongea na Kauli zenu wote zinakubaliana, vyote vinasema uwanja wa mpira mabpo mlishaanza kufanya maandalizi,” Alisema.
Kwa upande wake mkurugezi mtendaji wa hamshauri hiyo Palela Msongera amesema wamejipanga kuanza ujenzi huo mapema na kuwa tangu awali walikuwa wakisubiri mapendekezo ya eneo kutoka kwa wananchi kauli iliyoungwa mkono na mkuu wa wilaya hiyo Mh.Julieth Binyura.
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo inajumla ya vituo vya afya vinne hivyo kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia wananchi husani kutoka mwambao wa ziwa Tanganyika kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma za matibabu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa