• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Wangabo avitaka vyama vya Ushirika kujiepusha na madeni

imewekwa Tar: September 10th, 2019

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amevitaka vyama vya msingi vya ushirika mkoani Rukwa kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na wadau wa kilimo ikiwemo mabenki pamoja na wauzaji mbalimbali wa pembejeo ili wadau hao waweze kuendeleza uaminifu na hatimae kuwa na mahusiano mazuri yatakayoleta maendeleo ya wananchi katika mkoa.

Amesema kuwa kutolipa madeni chama kinajiweka katika mazingira ya kutokopesheka na wadau kukosa uaminifu hata kwa vyama vingine na kunasababisha wadau hao kushindwa kufikisha huduma kwa wakulima na hatimae kilimo kukosa tija, vyama vya ushirika kuyumba  na kuongeza kuwa dawa pekee ya kukopa ni kulipa.

“ Vyama vya Msingi vina madeni tena madeni makubwa, kwa mfanokuna kile chama cha Katazi AMCOS pamoja na Rukwa Farmers vyote vipo kule Wilaya ya Kalambo vinadaiwa shilingi milioni 395, vyama viwili sijajua kwengine lakini pale Mpui wanadaiwa Shilingi Milioni 485 au 490, lakini wao wamejipanga nilikuta mzigo mkubwa sana wa mahindi, tani zaidi ya 600, na waliniambia deni wanamaliza, lakini vile vyama viwili hata mahindi yaliyoko kwenye maghala yalikuwa hayazidi magunia 250 sasa watalipaje deni, ukiuliza wanasema kwamba hawakupata mavuno ya kutosha, lakini nje ya hapo wanauza” Alieleza.

Hivyo alitoa rai kwa vyama vya ushirika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwa kuchambua vyama vyote vinavyodaiwa, wadau wanaowadai, siku waliyokopa na siku wanayotakiwa kurudisha mikopo, aina ya mikopo,  walichorejesha tangu kukopa ili kuwa na orodha kamili na kuwafuatilia katika urejeshaji wa mikopo hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajenga Imani kwa wanaowakopesha na hatimae kukopesha zaidi.

Mh. Wangabo aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ufipa Cooperative Union Ltd (UCU) katika mkutano uliowajumuisha wadau wa kilimo katika mkoa ili kuona namna ya kuinua kilimo chenye tija pamoja na kuhuisha ushirika ndani ya mkoa.

Aidha, Wakati akiwasilisha mada yake kwa wakulima Meneja wa Benki ya Manedeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Dickson Pangamawe alisema kuwa viongozi wa shirika ndio nguzo ya wanaushirika, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wanachama wanafaidika na ushirika huo na kuhakikisha kuwa mikopo wanayoipata inawafikia wakulima wao.

“ Nyinyi ndio mtakaotujengea uamini kule kwa wakulima, sisi kama benki ya kilimo tuna fursa ya mikopo ya aina zote, kama wakulima wapo ‘serious’ na uongozi wao utasimama imara, tutawakopesha wataweza kufanya shughuli zao za kilimo bila ya shida yoyote, kwahiyo nitoe rai kwa viongozi wa ushirika, mara nyingi kumekuwa na shida na wakulima wanashindwa kuwa waaminifu kwasababu wanashindwa kusimamiana vyema katika vyama vyao, kwahiyo nyie muwe imara ili kuturuhusu sisi tuweze kuwawezesha,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Sumbawanga Abdillahi Nyangasa alishauri kuwa ili wakulima waweze kujikomboa alitaja mambo matatu makubwa ikiwemo Fedha, Masoko na Mkulima mwenyewe na kuongeza kuwa wao kama NFRA wanasimama katika kumhakikishia mkulima masoko na hivyo wakulima wanahitaji fedha za mikopo kutoka katika mabenki na wao kuwa tayari kutumia fedha hizo kwaajili ya manufaa ya kilimo chao.

“Mtazamo wa NFRA ni kuwafanya Wana Rukwa na Watanzania wengine tubadilike tuwe na uwezo wa kuuza bidhaa zetu za mazao ndani na nje ya nchi, bahati nzuri mkoa umeshaweza kulichukua hili na kulifanyia mkakati kwa maana ya ndugu zetu maafisa ugani, kazi ianzie shambani, tuna kiwango kikubwa sana tunachokipoteza cha mahindi tunayolima kwa hatua ya mwisho ya ubora, asilimia 30 mpaka 40 wakati mwingine mazao yanaharibika kwasababu ya kutozingatia kilimo chenye tija,” Alisitiza.  

Mkoa wa Rukwa una matrekta 124 yanayomilikiwa na wakulima binafsi hali iliyopelekea Mh. Wangabo kuvitaka vyama vya ushirika kusimamia kauli mbiu yao ya “ Ushirika, Pamoja tujenge uchumi” kwa kuanza na kumiliki matrekta ili kuwawezesha wanachama wao waweze kulima kwa tija na kuongeza mazao na sio kutegemea kilimo cha majembe au kutumia wanyama.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa