Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekabidhi kipeperushi kinachoelezea fursa zinazopatikana katika mkoa wa Rukwa kwa katibu mkuu wa jimbo la Kaskazini kutoka nchini Zambia ili kuweza kutangaza fursa hizo pindi atakaporudi nchini kwao.
Amekabidhi kipeperushi hicho katika kufunga kikao cha ujirani mwema kilichofanyika kwa siku mbili mkoani humo ili kufikia makubaliano ya pamoja “Memorandum of understanding” (MoU) ambapo rasimu ya makubaliano hayo iliandaliwa na kutegemewa kukamilika katika kikao kitakachofuata kitakachofanyika nchini Zambia mwaka 2019.
“kama tulivyofikia maamuzi mbalimbali, naziomba pande zote mbili ziweze kuandaa mpango kazi wa maazimio hayo kwaajili ya utekelezaji wa makubaliano haya, na nipende kuchukua fursa hii kumkabidhi kipepeprushi kinachoelezea fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa Katibu mkuu Mh. Elias Kamanga, kiongozi wa ujumbe kutoka Zambia ili kuweza kuzifahamu fursa hizo na kuzitangaza arudipo nchini kwao,” Mh. Wangabo alisema.
Nae Katibu huyo Mh. Kamanga alizitaka pande zote mbili kuhakikisha wanatimiza waliyoahidiana kwaajili ya manufaa ya leo na yajayo na ili kuimarisha udugu, umoja na mshikamano ulipo baina ya pande mbili za nchi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa