Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amezitaka halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wananunua chaki zinzotengenezwa na kiwanda cha kikundi cha “Perfect group” kilichopo Manispaa ya Sumbawanga ili kuweza kukuza soko la kiwanda hicho na kuthamini bidhaa za ndani ya mkoa ili kutoa fursa za ajira na kuinua kipato cha kikundi hicho.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi hundi zenye tamani ya shilingi 70,579,000 kwa vikundi mbalimbali 21 vya ujasilimali vikiwahusisha wanawake, vijana na walemavu iikiwa ni utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wa makundi hayo katika Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga ambapo Mh. Wangabo ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.
“serikali yetu ya wamu ya tano inasisitiza uanzishwaji na uimarishwaji wa viwanda vyetu vya ndani ili tupunguze kuagiza kutoka nje, sasa kama taifa tunalenga hivyo mkoa na wenyewe uko hivyo hivyo, nilazima tuhakikishe kuwa bidhaa zetu za ndani tunapatia soko ndani hapa hapa na kwa hali hiyo hizi chaki tunazotengeneza wenyewe katika mkoa wetu ni lazima zitumike katika halmashauroi zetu zote,” Alibainisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo Jacob Mtalitinya aliagiza kuwa shule zote zilizopo chini ya Ofisi yake kuhakikisha wananunua chaki kutoka katika kiwanda hicho ili kukuza soko na mtaji wa kikundi hicho pamoja na kuvitumia vikundi vya usafi katika kushiriki kuiweka manispaa safi na kununua matofali kwaajili ya majengo ya taasisi za serikali katika vikundi hivyo.
“Kiwanda cha chaki ambacho tunakipa mkopo leo, tunaelekeza na ninaelekeza tena shule zangu zote za manipaa tutanunua chaki zote kutoka katika kiwanda hichi kama utekelezaji wa masoko, lakini pia kwa upande wa usafi hatutaajili wakala vikundi hivi vitapewa kazi kwaajili ya usafi, wapo wanaofanya kazi za useremala na kazi nyingine tutaendelea kuwatumia kwenye kazi zetu za ujenzi kama utengenezaji wa “Ma-grill” kuhakikisha wanapata ajira na masoko na mitaji yao iweze kukua,”Alisema.
Shilingi 70,590,000/= inatolewa leo hii ili kuwezesha Vikundi 21 vya ujasiliamali amba 13 ni vya Wanawake 7 vya Vijana na 1 cha Walemavu.vikundi hivi vinajishughulisha na Usindikaji mafuta, chakula,vinywaji, Useremala, Utengenezaji wa Chaki na ushonaji, ufumaji na utengenezaji wa Mabatiki na Ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa