• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RUKWA KUPATA UMEME WA UHAKIKA : JIWE LA MSINGI LAWEKWA KATIKA MRADI MKUBWA

imewekwa Tar: July 29th, 2024



Mkoa wa Rukwa unatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dr.Dotto Mashaka Biteko, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia ambao utaunganisha Bara la Afrika kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.


Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi mradi huo wa TAZA iliyofanyika leo, Julai 29, 2024, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Kata ya Malangali, Mheshimiwa Dr. Biteko amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia takribani shilingi bilioni 15 kila Mwaka kununua umeme kutoka nchi jirani ya Zambia kwa ajili ya kuhudumia Mkoa wa Rukwa.


Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu amebainisha kuwa hatua ya kuunganishwa kwa Mkoa wa Rukwa katika gridi ya Taifa itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vya kuchakata na kusindika mazao hasa kwa kuwa Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo.


Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu ametoa maagizo kwa Mkandarasi wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) kuhakikisha kuwa umeme unawashwa katika vijiji 30 ambavyo bado havijafikiwa ifikapo Agosti 30, 2024.

Matangazo

  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MBIO ZA MWENGE ZAENDELEA KALAMBO RUKWA, MIRADI YA MAENDELEO YAENDELEA KUMULIKWa

    September 30, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAPOKELEWA MANISPAA YA SUMBAWANGA, MIRADI YA BILIONI 30.3

    September 29, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA AMALI WILAYANI NKASI; KIONGOZI ATAKA WANANCHI WATUMIE FURSA YA ELIMU YA UFUNDI

    September 28, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAPOKELEWA MKOANI RUKWA; KUKIMBIZWA KWA SIKU NNE; KUMULIKA MIRADI YA BILIONI 55.3

    September 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa