• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RUWASA Rukwa

imewekwa Tar: December 22nd, 2021

“WAKANDARASI TEKELEZENI MIRADI YA MAJI KWA UADILIFU” –

RC MKIRIKITI

Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji mkoani Rukwa wametakiwa kuwa waadilifu na wazalendo ili wananchi wapate maji vijijini na mijini kwa ustawi wa jamii hatua itakayo ondoa kero za ukosefu wa maji.

Kauli hiyo imetolewa leo (21.12.2021) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati aliposhuhudia hafla ya utiaji saini mikataba minne ya miradi ya maji kwa kati ya Wakala  wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na wakandarasi mjini Sumbawanga.

“Miradi hii haihitaji stori, tunahitaji siku 180 za mkataba zitumike kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji huku tukizingatia matumizi sahihi ya fedha pamoja na uadilifu “alisema Mkirikiti.

Katika hafla hiyo mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya shilingi 1,383,238,518 itakayotekelezwa kwa siku 180 katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga.

Akitoa taarifa kabla ya utiaji saini, Meneja wa Mkoa wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Boaz Matundali alisema jumla ya miradi 19 imetangazwa katika mwaka huu wa fedha ambapo minne kati yake imepata wakandarasi.

Mhandisi Boaz alitaja miradi itakayosainiwa kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji Msanda Muungano wilaya ya Sumbawanga wenye thamani ya shilingi Milioni 295.7 chini ya mkandarasi Kiluswa Building Contrators ya Sumbawanga.

Miradi mengine itatekelezwa katika wilaya ya Nkasi ambayo ni ujenzi wa mradi wa maji Lyazumbi  (shilingi Milioni 308.4), ujenzi wa mradi wa maji Kacheche (shilingi Milioni 385.0) na mradi wa maji Masolo (shilingi Milioni 395.9) yote itatekelezwa na mkandarasi Consel Construction and Engineering Services ya Mwanza.

Katika hatua nyingine Mhandisi Boaz alisema katika mwaka huu RUWASA mkoa wa Rukwa unatumia wakandarasi katika kutekeleza miradi yake tofauti na ilivyokuwa mwaka uliopita ambapo miradi ilitumia force account na nguvu za wananchi hivyo wanategemea itakamilika ndani ya kipindi cha siku 180 za mkataba.

“Kukamilika kwa miradi hii minne kutasaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji maji mkoa wa Rukwa toka asilimia 64 za sasa hadi kufikia asilimia 67 kwenye vijiji “alisisitiza Mhandisi Boaz.

Kwa upande wake mwakilishi wa wakandarasi Anyosisye Kiluswa aliishukuru serikali kwa kutoa kazi hizo kwa wakandarasi wazawa hatua itakayosaidia kukuza biashara na kuchangia upatikanaji ajira.

Kiluswa alitoa ahadi kuwa miradi hiyo wataitekeleza kwa ufanisi na ubora ili kuwezesha wananchi kupata maji kama serikali ilivyokusudia.

Naye Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Thomas Msuta alisema wanafuatilia kwa karibu miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha inakuwepo kwenye miradi hiyo.

“Sisi TAKUKURU tutafuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi hii ili fedha za serikali zitumike kwa usahihi kuhakikisha lengo la kuwezesha wananchi kupata maji “alisisitiza Msuta.

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa