RC MKIRIKITI: SERIKALI ITAKAMILISHA MIRADI YOTE KIPORO RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti leo (19.08.2020) alifanya ziara ya kuhamasisha wananchi kuendelea kufanya kazi kwa jitihada huku serikali ikiahidi kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi.
Ziara hiyo imemfikisha Mkuuhuyo wa Mkoa kwenye wilaya ya Nkasi ambapo amekagua miradi ya barabara, maji, elimu na afya iliyoibuliwa na kuanzishwa na wananchi.
"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha miradi yote kiporo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi inakamilika ndio maana imeendelea kutoa fedha za maendeleo" alisema Mkirikiti alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Kirando.
Kuhusu suala la elimu, Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka waongeze jitihada, ubunifu na uzalendo ili kiwango cha elimu kipande zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijuakali amesema wameweka mpango wa kuhakikisha miradi ya wananchi inakamilika ikiwa bora kwa kuzingatia maelekezo ya serikali
Lijuakali amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia kwa karibu kazi za wananchi ikiwemo miradi ya kipaumbele ikiwemo elimu na afya ili kero za wananchi zipate suluhu.
"Nimejipanga kwa ushirikiano na wakuu wa idara wa halmashauri kukamilisha kwa ubora miradi ya maendeleo huku tukihakikisha maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali tukiyatekeleza kwa haraka" alisisitiza Lijuakali.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa