Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere leo Agosti 17, 2024 amezindua shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika ambalo awali lilipumzishwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Mei 15, 2024.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezifungua shughuli hizo Mkoani Rukwa akimwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega ambaye awali alifanya zoezi kama hilo Mkoani Kigoma Agosti 15, 2024.
Sambamba na zoezi la uzinduzi wa shughuli za uvuvi, Mheshimiwa Makongoro amefanya kikao maalum na wadau wa uvuvi katika mwalo wa Kasanga, Wilayani Kalambo ambapo amekabidhi makasha 70 ya kuhifadhia samaki kwa wavuvi na wachakataji wa samaki.
Akizungumza katika hafla hiyo, RC Nyerere amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali kipindi Ziwa likiwa limepumzishwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa