Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imepongezwa kwa kutumia mfumo wa NeST katika kukamilisha manunuzi ya camera za cctv kwa ajili ya udhibiti wa upotevu wa mapato katika vizuizi vya barabarani wilayani humo.
Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2024, kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava wakati akizindua mradi wa kamera za kudhibiti utoroshaji wa mapato na mazao.
Ndugu Mnzava amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imetekeleza kwa vitendo maagizo ya Serikali kwa kufanya manunuzi kupitia mfumo wa NeST na hivyo kuzitaka taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi ikiwemo matumizi ya mfumo wa NeST.
Mwenge wa Uhuru Wilayani
Kalambo umezindua miradi 3, umeweka jiwe la msingi miradi 2 na kukagua miradi 3 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4.
Pamoja na miradi, viongozi wa mbio za Mwenge 2024 wametumia fursa hiyo kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Aidha Mwenge wa Uhuru Wilayani humo umewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji, kuzingatia lishe, kutokomeza UKIMWI na Kutokomeza Malaria.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa