• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

SITA WAFA KWA MATUKIO TOFAUTI IKIWEMO RADI

imewekwa Tar: February 18th, 2021

WANAFUNZI 6 wa shule mbalimbali za msingi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamefariki jana jioni ambapo Wanne walipigwa na radi na wawili kugongwa na gari katika maeneo tofauti,ambapo watatu kati ya waliopigwa na radi ni wa familia moja.

Akizungumza kwenye mazishi ya Watoto Watatu wa familia moja katika kijiji cha Nkana kata ya Nkandasi mkuu wa wilaya Nkasi Mh. Said Mtanda alisema kuwa wilaya Nkasi ina majonzi makubwa ambapo jana tu ni watoto 6 wamepoteza maisha ambapo Wanne walipigwa na radi na wawili kugongwa na gari katika maeneo tofauti.

Alisema kuwa vifo hivyo vimeleta simanzi kubwa wilayani Nkasi na kuwaomba Wananchi kuondoa fikra zozote mbaya juu ya vifo hivyo kwani yote ni mapenzi ya Mungu.

Awali kaimu afisa elimu wa wilaya Agnes Martin alisema kuwa licha ya Watoto watatu wa familia moja kuuawa kwa radi katika kijiji hicho cha Nkana pia kuna mwanafunzi mwingine wa shule ya msingi Nchenje naye alipigwa na radi wakati Wanafunzi wengine Wawili waligongwa na gari.

Aliwataja Watoto hao wa familia moja waliofariki kuwa ni Rita Remi Chiwalala (6) Mwanafunzi ya awali katika shule ya msingi Nkana,Macrida Chrisipine Mtepa (7) darasa la 1 na Exavery Lucas Chipamba (13) wa darasa la 5 na mwingine ni Kwilasa Siri (9) wa darasa la tatu shule ya msingi Nchenje ambaye alipigwa na radi jioni akiwa nyumbani kwao.

Pia aliwataja Wanafunzi wengine waliofariki kwa kugongwa na gari ni Boniphace Regius Sapi (8) wa darasa la pili shule ya msingi Kipundukala na Debora Chulula (12) darasa la tatu shule ya msingi Chala.

Akisimulia mkasa huo kaimu afisa elimu kata ya Sintali Patrick Fute alisema kuwa radi hiyo iliyowapiga Watoto wa familia moja ilitokea majira ya saa 11 jioni walipokuwa wakicheza mchezo wa kitoto na walikua 11 na baada ya radi hiyo kushuka Watoto hao watatu walifariki papo hapo.

Na Israel Mwaisaka,Nkasi

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa