Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Rukwa imeendelea kutoa elimu kwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2024 mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Bw. Mzalendo Widege amesema kuwa lengo la kuendelea kutoa elimu ni kuhakikisha uwepo wa uwazi uwajibikaji na ufanisi katika usimamizi wa miradi yote inayopokea fedha toka Serikalini na ile inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo.
Taarifa hiyo ya utekelezaji kazi wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa imetolewa tarehe 27 Agosti 2024 ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wa taasisi hiyo kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu kila mwezi.
Pamoja na taarifa hiyo Kamanda Mzelendo ametumia fursa hiyo kueleza mikakati ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa kipindi cha mwezi Septemba na kuendelea. Amesema wasimamizi wanafundishwa kuvitambua viashiria vya rushwa na kuviepuka.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa