• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

TARURA

imewekwa Tar: September 9th, 2022

BILIONI 12 KUBORESHA BARABARA ZA TARURA RUKWA


Na. OMM Rukwa


Serikali ya Awamu ya Sita imeupatia mkoa wa Rukwa shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mikataba 29 ya ujenzi na matengenezo ya barabara kati ya TARURA na wakandarasi leo (07.09.2022) mjini Sumbawanga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga alisema fedha zilitolewa  zinatokana na mfuko wa barabara na tozo ya mafuta.

Sendiga aliwataka wakandarasi hao kwenda kutekeleza mikataba ya ujenzi na ukarabati wa barabara za vijijini na mitaani kwa weledi na ubora wakizingatia kuwa fedha za watanzania ndizo zinatekeleza miradi hiyo.

“Tuna fedha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2022/23 kati hizo Bilioni Tano zimetokana na tozo ya mafuta kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara hizi. Sasa lazima tukazifanyie kazi ili wananchi wapate manufaa ”alisema Sendiga.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo kwa wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya miezi sita ya mkataba na kuwa hatopenda kusikia mkandarasi akiomba nyongeza ya muda wa kukamilisha mradi.

Akitoa taarifa kwenye hafla hiyo, Meneja wa TARURA Rukwa Mhandisi Samson Kalesi alisema jumla ya mikataba 29 yenye thamani ya shilingi Bilioni Sita  kwa awamu ya kwanza imesainiwa kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwenye halmashauri nne za Rukwa.

Mhandisi Kalesi alitaja shughuli zitakazofanyika kuwa ni ujenzi wa barabara mpya za lami (km 0.5) zitajengwa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, (km 1.5) zitajengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.

Aidha Mhadisi Kalesi aliongeza kusema kuwa (km 265.95) zitajengwa kwa kiwango cha Changarawe, (km 140.01) zitafanyiwa matengenezo ya maeneo korofi , (km 220.22) zitafanyiwa matengenezo ya kawaida na makaravati 67 na madaraja matatu yatejengwa.

“Leo tunashuhudia utiaji saini wa mikataba  29 kati ya TARURA na wakandarasi yenye jumla ya Shilingi 6,182,956,557.60 kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na makalavati, mikataba hii ni ya awamu ya kwanza ambayo ni sawa na asalimia 60% ya kazi zote zitakazo tekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023” alisema Mhandisi Kalesi.

Kwa upande wake mwakilishi wa wakandarasi mkoa wa Rukwa Gaudence Kipesha alisema wanaipongeza TARURA kwa kuandaa mikataba inayoeleweka na yenye uwazi tofauti na miaka ya nyuma na kuwa wataenda kuitekeleza kwa ubora na kuzingatia muda uliokubalika .

TARURA Mkoa wa Rukwa inahudumia barabara za lami zenye urefu wa kilometa 41.817, changarawe zenye urefu wa kilometa 847.18 na barabara za vumbi zenye urefu wa kilometa 1418.66

Mwisho.

 

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa