Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Kalambo wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo pamoja na Halmashauri zote, kushirikiana pamoja katika kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji hasa yale yanayopeleka maji yake katika maporomoko ya mto Kalambo ili kuweza kutunza eneo hilo linalotarajiwa kuiingizia serikali mapato kutokana na utalii.
Kaimu meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Chesco Lunyungu ameyasema hayo baada ya kutembelewa na msafara wa Mkuu wa Mkoa uliokwenda kwenye maporomoko hayo kujionea utekelezaji wa uimarishaji wa ujenzi wa ngazi unaoelekea maji yanapodondokea ili kuwarahishia watalii kuweza kufika katika eneo hilo kwa urahisi.
“Tunaomba wananchi wote wanoishi katika vijiji ambavyo maji haya yam to kalambo yanatoka tuwahamasishe wananchi wote kwa kushirikina na Halmashauri zetu tuendelee kuhifadhi mazingira, kwasababu maporomoko haya yanategemea sana maji na maji yanategemea uhifadhi wa mazingira kwa hiyo kutoweka kwa mito hasa mto Kalambo kutasababisha kupoteza rasilimali hii na kupoteza watalii,” Alisema.
Katika Kuhakikisha jambo hilo halifumbiwi macho nae Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema kuwa kadiri miaka inavyozidi kwenda ndipo maji hayo yanapungua endapo mazingira hayatahifadhiwa hivyo alitoa rai kwa wananchi.
“Nitoe rai kwa wananchi wote wa maeneo haya kutunza na kuhifadhi mazingira watu wasikate miti hovyo na wasijishughulishe na jambo lolote ndani yam situ huu wauwache huu msitu kamaulivyo na tutakuwa wakali sana kwenye utunzaji wa mazingira, hatutaki kupoteza haya maporomoko ambayo yanasifa kubwa katika nchi yetu, tutahakikisha mtu yeyote ambaye anaharibu mazingira tutamchukulia hatua kali sana za kisheria, kama kuna mtu yeyote analeta usumbufu TFS tuambiane ili tushirikiane bega kwa bega, vijiji vyote tutavipa elimu ili kutunza mazingira na kulinda utajiri huu,” Alimazia.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa