• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

TUME YA UCHAGUZI YAZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA MPIGA KURA KUZINGATIA SHERIA NA MAELEKEZO

imewekwa Tar: July 31st, 2025

Taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu zimetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume  na taasisi na asasi hizo  leo Julai 30, 2025 jijini Dar es Salaam. ”Nitoe rai kwenu haswa wale mliopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo la kutoa elimu ya mpiga kura,” amesema Jaji Mwambegele. 

Amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura. ”Niwaombe msichoke kuwasisitiza na kuwahimiza wadau na wananchi kwa ujumla kuzingatia Sheria za Uchaguzi, Kanuni na Maelekezo ya Tume. Tume nayo kwa upande wake itaendelea kuzingatia Sheria za Uchaguzi na Kanuni katika michakato yote ya uchaguzi,”amesema. Jaji Mwambegele ameongeza kuwa wakati wa kampeni uzoefu unaonesha kuwa kunakuwa na joto la kisiasa linatokana na baadhi ya watu kukosa uvumilivu wa kisiasa, hivyo ameziasa taasisi na asasi hizo kutumia nafasi yao kuwaelimisha wananchi ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu. ”Kipindi hicho cha kampeni mnapaswa kuwahimiza wananchi kupitia majukwaa yenu kuwa makini kwa kuhakikisha kuwa hawawi chanzo cha kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema. 

Kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(g)(h) na (i) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, Tume inao wajibu wa kutoa elimu ya mpiga kura nchini,           kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa elimu ya mpiga kura na kualika na kusajili waangalizi wa uchaguzi. Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kwa  taasisi na asasi 164 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na  taasisi na asasi 76 za ndani na 12 za kimataifa zimepata kibali cha uangalizi wa uchaguzi. Baadhi ya wawakilishi wa taasisi na asasi hizo wamesema wamejipanga rasmi kutoa elimu ya mpiga kura haswa kwa vijana wanaotarajia kupiga kura kwa mara ya kwanza.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA - 2025, KULINGANA NA MATOKEO YALIYOTANGAZWA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) June 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TUME YA UCHAGUZI YAZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA MPIGA KURA KUZINGATIA SHERIA NA MAELEKEZO

    July 31, 2025
  • RUKWA YAENDELEA KUCHUKUA HATUA THABITI KUDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    July 28, 2025
  • RUKWA YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU JUMUISHI YA TAIFA YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

    July 24, 2025
  • INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UCHAGUZI KUZINGATIA VIAPO VYAO NA MAADILI YA KAZI

    July 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa