• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Ugawaji Hati Hakimiliki za Kimila

imewekwa Tar: October 27th, 2022

LEAT NA RUSUDEO WATOA HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA 4,530 NKASI

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amepongeza Timu ya Wanasheria Watetezi wa  Mazingira kwa Vitendo  (LEAT) na Shirika la Maendeleo Endelevu Rukwa ( RUSUDEO) kwa kufanikisha utoaji wa Hati Za Haki Miliki za Kimila 4,530 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Tambaruka, Lyele na Kisula wilaya ya Nkasi.

                 

Pongezi hizo amezitoa leo (Oktoba 26,2022) wakati akizindua zoezi la ugawaji hati hizo kwenye kijiji cha Tambaruka ambapo amesema zinakwenda kuwa msaada kwa wananchi kiuchumi pamoja na kusaidia kuondosha migogoro ya ardhi.

"Naomba viongozi wa ngazi zote kuanzia wenyeviti wa vitongoji, vijiji na madiwani shirikianeni na LEAT ili kutoa elimu  kuhusu faida za hati za haki miliki za kimila ili zoezi lisipotoshwe na watu wasiotakia mema wananchi. LEAT hawajaja kupoka ardhi yenu bali wamekuja kupima na kuwapa hati miliki za kimila na ardhi ni umiliki wenu" alisema Sendiga.

Kwa upande Msimamizi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili Bi. Hana Lupembe alisema mradi huo wa miaka mitano ulianza mwaka 2020 hadi 2025 umenufaisha vijiji 18 katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga.

Mratibu huyo alitaja mafanikio mengine ni pamoja na kuwezesha halmashauri utengaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 13 kati ya 18 sawa na asilimia 86 ya lengo na pia wametoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi 2,170 kati ya lengo la kuwafikia watu 1,798.

Mradi huo wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili unatekelezwa na LEAT pamoja na RUSUDEO kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani ( USAID) ambapo katika uzinduzi wa leo umehudhuriwa na Bw. Colin Dreizin ambaye ni Mkurugenzi wa Kukuza Uchumi USAID Tanzania.

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa