• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

UMOJA NA MSHIKAMANO SILAHA ZA MAFANIKIO MIAKA 62 YA UHURU

imewekwa Tar: December 9th, 2023

Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa mafanikio yaliofikiwa na Tanzania kwa kipindi cha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara hayakuwahi kufikiwa na wakoloni kwa kipindi cha miaka 77 ya ukoloni.Ametaja umoja na mshikamano kuwa silaha zilizoifanikisha Tanzania katika miaka 62 .

Mheshimiwa Makongoro Nyerere ameyasema hayo leo tarehe 09 Desemba  2023, wakati wa maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kalambo.


Akifunga mdahalo wa kujadili mafanikio yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali katika kipindi cha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta za  Afya, Elimu, Miundombinu, Kilimo, Siasa, Teknolojia na Nishati.

Ameeleza kuwa mpaka kufikia tarehe ya maadhimisho ya Mwaka huu 2023, vijiji 289 kati ya 339 vya Mkoa wa Rukwa vina umeme.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Sekta ya Afya imeendelea kuimarika na kuwa idadi ya Hospitali kwa Mkoa wa Rukwa inafikia Hospitali 7,  vituo vya Afya 25 na Zahanati 219 wakati idadi ya shule za Msingi ikifikia 401, Shule za Sekondari 112 vyuo vya kati 14 na vyuo Vikuu 2.


Amesema kuwa mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na umoja na mshikamano uliokuwepo kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza hadi Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan.


Mheshimiwa Makongoro amewaomba wananchi wasikubali kugawanywa kwa rangi, ukabila, dini au kwa namna yeyote ile  bali wazilinde tunu za Taifa na  misingi imara iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa la Tanzania.


Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa