RC MKIRIKITI: "WANA RUKWA JITOKEZENI KUPATA CHANJO YA UVIKO 19 NI SALAMA "
Wananchi wa mkoa wa Rukwa wamehamasishwa kujitokeza kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo serikali mkoa wa Rukwa imeanza kutoa chanjo kwa wananchi wenye utayari na hiari .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti leo (04.08.2021) amewaongoza wananchi wa mkoa huo kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo amesema kuwa chanjomhiyo ni salama na inalenga kuwasaidia watu kuwa na kinga imara .
Mkuu huyo amewaeleza wakazi wa Sumbawanga waliokusanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kuwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhibitisha pasipo shaka kuwa chanjo hii ya UVIKO 19 ni salama na kuwa wengi wajitokeze kupata chanjo.
"Rais Samia amesema chanjo hii ni bure na ya hiari kwa mwananchi yeyote mwenye kuhitajinili kujikinga na ugonjwa wa Corona. Mimi leo nitakuwa wa kwanza kuchanja hapa hapa " alisema Mkirikiti
Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi wa serikali na dini , wazee maarufu pamoja na wananchi toka wilaya zote za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo wananchi wengi wamehamasika kupata chanjo hiyo.
Mkirikiti ameto agizo kwa wakuu wa wikaya kutoa elimu kwa kushirikiana na viongozi wa dini juu ya kudhibiti mikusanyiko na kwenye shughuki za misiba ili kuepuka maambukizi kusambaa.
Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza wataalam wa afya kutoa elimu ya kujikinga ikiwemo umuhimu wa kufanya mazoezi hatua itakayosaidia kuongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.
Akizungumza kuhusu chanjo hiyo Mganga Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema lengo la serikali kutoa dozi hizo za chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona utasaidia kuongeza kinga ya mwili ya mwanadamu .
Aliongeza kusema lengo jingine ni kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa pia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona.
" Tumepokea dozi za chanjo Elfu Ishirini ambazo tayari zimefikishwa kwenye vituo 11 vilivyoanishwa kutoa chanjo, wananchi naomba tujitokeze kupata chanjo" alisema Dkt. Kasululu
Naye Mzee maarufu wa Sumbawanga Kapteni Mstaafu Nkoswe Noel (81) amefurahi kupata chanjo hiyo na kuiomba serikali kuwafikishia wananchi wengi chanjo ili waepukane na ugonjwa huu hatari wa korona.
Mzee Nkoswe amewasihi wakazi wa Rukwa kujitokeza na kuchanja ili maradhi ya Corona yasiendelee kuenea nchini na kuongeza kuwa serikali ilete chanjo zaidi ya 20,000 za sasa.
Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Rukwa Rashid Akilimani akizungumza baada ya kupata chanjo ya UVIKO 19 alisema ameshukuru kupata dozi hiyo kwani itamwezesha mwaka huu kwenda kutekeleza ibada ya Hija.
" Mwaka jana 2020 sikuweza kwenda Hija nchini Saudia baada ya kukosa chanjo ya UVIKO. Leo ninashukuru serikali kutuletea chanjo hii hapa Rukwa" alisema Sheikh Akilimali.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa