• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Viongozi Rukwa waendelea kuhamasisha matumizi ya Nyungu

imewekwa Tar: May 3rd, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa wito kwa wananchi na wadau wote mkoani humo kuhakikisha wananchukua hatua za tahadhari ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya pamoja na kushauri matumizi ya Nyungu kwaajili ya kujifukiza.

Amehamasisha hayo ikiwa ni katika kuunga mkono kauli ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na viongozi wengine wa juu nchini katika kupambana na Covid – 19 ambao huenezwa kwa kuingiwa na majimaji yatokayo kwa njia ya hewa wakati mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya au kugusa majimaji yanayotoka puani mwa mtu aliyeathirika.

“Nitoe wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na nyini waheshimiwa madiwani kuchukua hatua za tahadhari ya ugonjwa huu kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wetu wa afya. Tukumbuke kuwa virusi vya Corona ni janga la kidunia na linaua, Aidha matumizi ya Nyungu kwaajili ya kujifukizia yanashauriwa na Mh. Jafo waziri wa OR-TAMISEMI pamoja na viongozi wengine wa juu tuyazingatie, watu wapige Nyungu,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia anakaimu Wilaya ya Sumbawanga Mh. Said Mtanda akifafanua michanganyiko ya aina tatu inayoshauriwa na wataalamu wa tiba ya asili yaliyofanyiwa majaribio na kituo cha Tiba asili kinachotambulika na serikali amesema moja ya mchanganyiko ni kutumia mti wa mwarobaini, tangawizi iliyopondwa, majani ya mpera, limao zilizokatwa  unachemsha pamoja na kisha kujifunika na kuvuta moshi kwa pua na mdomo ili moshi huo uingie mwilini na hatimae kwenda kuua virusi vya Corona.

“Sisi kule Namanyere tumeweka utaratibu wa kuhamasishana kujifukiza, kwasababu ukiona aibu matatizo kweli utayapata, kwahiyo kiongozi ukiwa unajifukiza unakapiga kapicha kidogo unawatumia wengine ili waseme hee hata Diwani kajifukiza, kwahiyo wale unaowaongoza watahamasiska kujifukiza kwasababu wataona kumbe sasa hili sio suala la aibu,” Alisema.

Viongozi hao wamesema hayo wakati wa vikao vya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na Wilaya ya Sumbawanga katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri hizo kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MADAKTARI BINGWA 33 WAPOKELEWA RUKWA, HUDUMA ZA KIBINGWA KUTOLEWA HOSPITALI ZA WILAYA KWA SIKU TANO

    May 19, 2025
  • RUKWA YAANZA RASMI MATUMIZI YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA ZAO LA MBAAZI NA UFUTA

    May 13, 2025
  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa