Vyama vya ushirika vinavyojihusisha na mazao ya mahindi na mpunga Mkoani Rukwa vimenufaika na mkopo wa shilingi Bilioni 2.1 kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024.
Mrajis Msaidizi, Bw Marton Bafuta Mtindya ameyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya ushirika Mkoani Rukwa katika maadhimisho ya Siku ya Ushirika Mkoani Rukwa leo tarehe 05, Juni 2024.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Ushirika yaliyoandaliwa na Jukwaa la Ushirika yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Moravian ulioko Sumbawanga.
Mheshimiwa Peter Ambrose Lijualikali, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi amevipongeza vyama vya ushirika Mkoani Rukwa kwa kuchangia ukuaji wa Sekta ya Ushirika. Amesema amefurahishwa na utekelezaji wa kipaumbele cha sita kati ya vipaumbele saba vya Ushirika ambacho ni ushirikiano miongoni mwa vyama vya Ushirika.
Mheshimiwa Lijualikali amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Rukwa kuhamasisha na kutoa elimu ya ushirika kwa wananchi.
Mheshimiwa Lijualikali amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika Siku ya Ushirika Mkoani Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa