• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Waalimu wastaafu Mkoani Rukwa wadhulumiwa zaidi ya Shilingi milioni 96 fedha za SACCOS

imewekwa Tar: June 12th, 2020

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameshangazwa na kitendo cha waalimu wastaafu wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) mkoani humo kudhulumiwa shilingi 96,456,250/= badala ya kuwa mfano wa kuigwa kutokana na kuwa mstari wa mbele katika kudai haki zao pamoja na kuongezewa mishahara kutoka serikalini.

Amesema kuwa inashangaza kuona waalimu hawa wenyewe kwa wenyewe kwenye vyama vyao wanadhalilishana na kunyayasana badala ya SACCOS zao kuwa za kuigwa kutokana na kuzisimamia wenyewe na sio kudhulumiana huku wengine wakiwa na hali mbaya kiuchumi na hivyo kuwataka viongozi wa vyama hivyo kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa misingi ya sheria.

“Hizi SACCOS za waalimu zinapaswa kuwa za mfano wa kuigwa, kwasababu zinasimamiwa na wao wenyewe, lakini hapa tunaona kabisa kwamba waalimu tena wastaafu ‘wanapigwa’, wengine wana hali mbaya, wamedhalilishwa na kunyanyaswa kwa muda mrefu, viongozi wa vyama hivi vya SACCOS lazima muwe waadilifu,” Alisisitiza.

Aliongeza kuwa mkoa upo katika harakati za kuimarisha vyama vya ushirikia na lengo hilo halitafikiwa endapo kutakuwepo na viongozi wabovu, wasiofaa, ambao hawajali maslahi ya wanachama wao, amabao ndio wametufikisha hapa mpaka tukawaagiza TAKUKURU wawashughulikie hao viongozi.

Wakati akichanganua mgawanyo wa fedha hizo katika taarifa ya ubadhilifu huo Mkuu wa Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Rukwa Hamza Mwenda alisema kuwa shilingi 56,700,000/= zitarejeshwa kwa Waalimu Wastaafu 39 wa SACCOS ya CHAUWAMI ambayo inahusisha waalimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Kalambo

Pia alisema kuwa Shilingi 39,756,250/= zitakabidhiwa kwa viongozi wa Nkasi Teachers SACCOS. Shilingi 1,345,000/= zitarudishwa kwa kwa SACCOS ya MAKUPA iliyopo wilayani Nkasi ikiwa ni fedha ambazo zilikopeshwa kwa wananchama lakini wakagoma kuzirejesha kwenye SACCOS kwa mujibu wa masharti ya muda wa marejesho ya mikopo yao.

“Uongozi wa awali wa SACCOS ya Nkasi Teachers uliandaa nyaraka na kuwakopesha watu wasio wanachama kinyume cha sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya Mwaka 2013. Uchunguzi huu ulitokana na taarifa ya COASCO ambayo waziri wa Kilimo alimkabidhi Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU kwaajili ya kuifanyia kazi, fedha hizi zimerejeshwa na leo tutaomba uwakabidhi viongozi wa Nkasi Teachers SACCOS na zitaingizwa katika akaunti ya chama leo,” Alieleza.

Akiongea kwa niaba ya waalimu wenzie Mwalimu Mstaafu Benard Mpepo alitoa shukrani kwa serikali kwa kuwa na chombo thabiti cha kutetea haki za wanyonge na kubainisha kuwa haki hiyo ilikuwa ngumu kuipata lakini kutokana na umakini wa chombo hicho hatimae wamepata haki yao

Makabidhiano hayo yametokea jana (11.6.2020) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi fedha hizo kwa waathiriwa wa vitendo vya rushwa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo na kuhudhuriwa na waalimu wastaafu na watumishi wengine wa serikali wa Idara za Ulinzi na Usalama.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa