Katibu tawala msaidizi serikali za mitaaa wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya amewaasa watumishi wapya wa kada wa uhasibu katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria, taratibu na miongozo inayotolewa ili kuwaepusha kufanya kazi kwa mazoea.
Ameyasisitiza hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya uhasibu katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma (FFARS) akimuwakilisha AKtibu Tawala wa Mkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa
“Ni matumaini yangu kuwa baada ya mafunzo haya mtakuwa mmejenga uelewa wa kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka mbalimbali,” Alisema.
Aidha mafunzo hayo yamelenga kuwaboreshea ujuzi na stadi za kazi ikiwemo dhana ya kwenda na mahitaji ya wakati kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Technolojia.
Mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waajiriwa wapya wahasibu wasaidizi katika halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Sumbawanga vijijini, Nkasi na Kalambo, walioambatana na maafisa utumishi pamoja na maafisa takwimu wa Halmashauri hizo.
Pamoja na mafunzo hayo watumishi hao wapya walipata fursa ya kueleimishwa kuhusu mifuko mbalimbali ya jamii ikiwemo, PSPF, LAPF, NSSF, na mfuko wa bima ya afya wa Taifa (NHIF) ili kuwapa nafasi watumishi hao wapya kuamua kwa hiari bila ya kulazimishwa mfuko ambao watapenda kujiunga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0739862632
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa