SERIKALI KUTHIBITI UUZAJI NA USAMBAJI WA MBOLEA KWA MFUMO WA KIDIGITALI.
Mawakala na wauzaji wa mbolea mkoani Rukwa wamepatiwa mafunzo na Mamlaka ya Uthibiti Mbolea Tanzania (TFRA) namna ya kuagiza na kusambaza mbolea kupitia mfumo wa kidigitali ambao Serikali imeuandaa kwa lengo la kuthibiti Uingizaji na Usambazaji wa Ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa mwaka 2022/2023.
Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania Dkt. Stephen Ngailo amesema lengo la mfumo huo ambao unapatikana Katika Play Store kwa kupakua programu inayoitwa TFRA AGRODEALER TOOL ni kupata taarifa za kila siku za uuzaji na Usambazaji wa Mbolea, Kuepusha Wizi,kupunguza mda wa Kuagiza mzigo,kutambua wakulima na wauzaji kwani mfuko mmoja utauzwa kwa mara moja tu.
Kikao hicho cha wadau wa pembejeo za ruzuku kimefanyika (27.08.2022) katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mjini Subawanga na kuhusisha wafanyabiashara wa mbolea na wawakilishi wa wakulima .
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala msaidizi sekta ya uchumi na uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Malabeja Rogate amewataka amewataka wasambazaji wa Ruzuku ya Mbolea kuzingatia maelekezo ya TFRA na Serikali kwa ujumla Katika kuingiza na kusambaza Mbolea.
Aidha Rogate amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika msimu wa Kilimo 2022/2023 unameweza kutenga bajeti ya kutosha ya kununuliwa mbolea na kuwataka wakulima kujiandaa kushiriki Kilimo.
Kwa Upande wake washiriki wa mafunzo ya namna ya kujisajili kwenye mfumo wa kidigitali wamepongeza namna mfumo huo kuwa unaenda kurahisisha zoezi la uagizaji mbolea Hali itakayopunguza pia mianya ya wna kumwezesha wakala wa mbolea kuagiza Mbolea kulingana na mahitaji ya wakulima.
Mbolea zitakazohusika kwenye ruzuku ni mbolea ya DAP kwa ajili ya kupandia na UREA kwa ajili ya kukuzia ambazo ni takribani asilimia 50 ya matumizi ya mbolea nchini.
TFRA imesema kigezo muhimu cha wakulima kusajiliwa ili kupata mbolea ya ruzuku ni kuwa na shamba ambapo wanatakiwa kwenda katika ofisi za vitongoji, mtaa au kijiji mahala wanapolima wakiwa na kitambusho cha Taifa au cha Mpiga Kura kisha watasajiliwa.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa