Mamia ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za matibabu za kibingwa zinazoendelea kutolewa na katika hospitali zote za Wilaya Mkoani Rukwa, wameipongeza Serikali kwa mpango wa kusogeza huduma hizo katika ngazi za Wilaya.
Bi. Lydia Mwananjela Mkaazi wa Wilayani Nkasi na Bw Ayub Mlwafu Mkaazi wa Manispaa ya Sumbawanga wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mpango huo wakieleza kuwa umepunguza kwa kiwango kikubwa umbali na gharama za kufuata huduma za kibingwa.
Wakizungumzia mpango huo wa huduma wataalam wa Afya Wilaya Nkasi wameipongeza Serikali kwa kuwapa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa