• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Wananchi Rukwa kushiriki kuchangia Damu kusaidia Majeruhi ajali ya Morogoro

imewekwa Tar: August 13th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa mkoa huo kushiriki katika zoezi la kuchangia damu litakalofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 14 hadi 18.8.2019 katika halmashauri nne za mkoa, ili kusaidia majeruhi walioungua na moto uliosababishwa na kulipuka kwa lori la Mafuta katika ajali iliyotokea eneo la Msavu mkoani Morogoro, na kusababisha vifo vya watu 76 na majeruhi 54.

Mh. Wangabo amesema kuwa zoezi hilo litawajumuisha Waendesha Bodaboda na Bajaji, Madereva wa Magari, Vijana, Watumishi wa Serikali, Wanafunzi, Vyama za Siasa, Madhehebu ya Dini, Viongozi mbalimbali na wale wote wenye mapenzi mema na moyo wa kujitolea kwaajili ya majeruhi hao.

“Nafahamu kuwa mtu yeyote aliyeungua sehemu yoyote ya mwili, miongoni mwa madhara makubwa anayoyapata ni pamoja na kupoteza kiasi kikubwa cha maji mwilini (Dehydration) na kupungukiwa damu mwilini (Anaemia).  Kwa hiyo natoa wito na kuwaomba Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuchangia Damu kwa ajili ya wenzetu majeruhi wanaoendelea na matibabu.  Damu hiyo pamoja na salamu zetu za pole tutaiwasilisha kwa Dkt. Kebwe Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,” Alisema.

Aidha Mh. Wangabo kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa anaungana na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Viongozi wa Mkoa huo, Familia za Marehemu, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Wapendwa wao.  Na kumuomba Mwenyezi Mungu awape Moyo wa Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Mungu awape pumziko la milele waliopoteza uhai na awaponye Majeruhi wote wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.  ‘Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa Jina lake lihimidiwe’.” Alimalizia.

Mh. Wangabo ametoa maelekezo hayo kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kilichohusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa