• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Wanaowinda panya washauriwa kufuga kuku ili kupunguza uharibifu wa mazingira.

imewekwa Tar: January 21st, 2019

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewashauri wananchi wote wanaoharibu misitu kwa kuchoma moto kwaajili ya kuwinda panya waanze kufuga kuku ili kuweza kuokoa mazingira huku

akiwataka wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wanamuandalia mipango mikakati ya halmashauri zao katika upandaji wa miti ikiwa ni kufuata agizo la serikali la kuitaka kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Alisema kuwa moja ya matokeo ya shughuli hizi za kibinadamu ni uharibifu mkubwa wa mistu na vyanzo vya maji  unaoweza kusababisha madhara makubwa kama kukosa mvua kwa wakati, uzalishaji mdogo wa chakula na hata maradhi mbalimbali yanayotokana na uharibifu wa mazingira na kuongeza kuwa ufanisi wa zoezi hili la upandaji miti unatia shaka kutokana na kutosimamiwa vizuri na Viongozi wa Halmashauri zetu zote.

“Kwa hiyo naagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri zetu kuwasilisha mpango mkakati wa upandaji miti kwa kipindi cha Mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kubainisha idadi ya miti waliyonayo na mahali ilipo pamoja na ya Wadau wao wa utunzaji wa Mazingira, na maeneo ya kupanda.  Mpango huu unifikie ndani ya siku tano kuanzia leo,” Alisisitiza.

Vile vile alizitaka Taasisi za Serikali kama shule, magereza na vyuo vya elimu kuanza kutumia nishati mbadala ikiwemo ya “biogas” katika shughuli zao za mapishi ya chakula na kupunguza kasi ya matumizi ya kuni kwani mkoa una mitambo 2 ya “biogas” katika Manispaa ya Sumbawanga katika Vijiji vya Mtimbwa na Ntendo ambayo inatumika kama darasa la kujifunzia  ujuzi wa kutengeneza biogas kutokana na mabaki ya mifugo yetu.

Wakati akisoma taarifa ya halmashauri juu ya zoezi la upandaji miti, Afisa Ardhi na malisili wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Juma Chande alieleza kuwa katika msimu wa mwaka 2018/2019 katika kata 8 kati ya kata 27, halmashauri imeshapanda miti 292,899 ambayo ni asilimia 17.4 ya lengo na ufafanua kuwa halmashauri inaendelea kutoa elimu ya kutunza mazingira, kupanda miti na kilimo mseto huku akitaja changamoto zinazorudisha nyuma juhudi hizo.

“Miongoni mwa changamoto ni muitikio mdogo wa wananchi katika utunzaji wa mazingira pamoja na hamasa nyingi kutolewa kwao, mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya mathalani kusababisha uchomaji wa miti wakati wa kiangazi mfano maeneo ya vijiji vya Msandamuungano, Sandulula na Mpwapwa hivyo kuathiri misitu iliyopandwa.” Alimalizia.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa