• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Watendaji Wasihamishwe Wakiharibu

imewekwa Tar: November 9th, 2022

MARUFUKU MTENDAJI KUHAMISHWA AKIHARIBU MRADI :

RC SENDIGA

 

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa Rukwa Queen Sendiga ameagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa kuchukua hatua za kuwarejesha watendaji na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuharibu miradi ya wananchi ili wajibu tuhuma zao.

Kauli hiyo ameitoa jana (Jumatatu, Novemba 07, 2022) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kabwe wilaya ya Nkasi ambapo walilalamika kuwa Mtendaji amehamishwa baada ya kuharibu mradi wa zahanati.

Mkuu wa Mkoa huyo alitembelea zahanati ya kijiji cha Kabwe na kujionea hali ya kukwama kwa ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo linadaiwa kupatiwa vifaa vya mabati na saruji toka kwa wafadhili mwaka 2020 lakini halijakamilika.

“Mtendaji wa Kata aliyekuwa hapa arejeshwe kuja kutoa majawabu ya tuhuma za kutokamilika zahanati ya kijiji cha Kabwe wakati vifaa vya ujenzi vilitolewa na wafadhili” alisema Sendiga.

Katika hatua nyingine Sendiga ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo na kwa wahusika watakaobainika hatua za kisheria zichukuliwe haraka.

Kwa upande wake Diwani Kata ya Kabwe Asante Lubisa alikiri kupokelewa kwa vifaa vya ujenzi wa zahanati hiyo toka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mwaka 2020 lakini kutokana na ramani iliyopangwa kubadilika mradi umeshindwa kukamilika hadi sasa.

Mkuu wa Mkoa huyo akiwa wilayani ya Nkasi alikagua kituo cha Afya Kasu, Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa madarasa sekondari ya Kabwe na bandari ya Kabwe ambapo alisema hatokubali kuona miradi ikisua sua.

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • REA KUANZA KUSAJILI NA KUUZA MAJIKO BANIFU MKOANI RUKWA

    August 28, 2025
  • MPANGO BORA WA UFUGAJI NYUKI WAWAFIKIA MACHIFU RUKWA

    August 20, 2025
  • TUME YA UCHAGUZI YAZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA MPIGA KURA KUZINGATIA SHERIA NA MAELEKEZO

    July 31, 2025
  • RUKWA YAENDELEA KUCHUKUA HATUA THABITI KUDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    July 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa