Wazazi Mkoani Rukwa wametakiwa kuwapatia watoto wao wa kike elimu kuhusu hedhi salama ili kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kusababisha ugumba.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa walimu na wazazi juu ya hedhi salama, Bi Sabina Songela ambaye ni Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, amesema elimu ya hedhi inalenga pia kuwasaidia watoto wa kike walio wanafunzi kupata nafasi ya kuhudhuria darasani siku zote za mwaka.
Mafunzo hayo ya hedhi salama yanayowahusisha walimu na wazazi kutoka wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga yamefinguliwa leo tarehe 02 Juni 2023. Mafunzo hayo yanatolewa kwa shule zote zinazotekeleza miradi ya SWASH.
Amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kutenga muda kwa ajili ya kuzungumza na kuwafundisha watoto wao kuhusu hedhi salama na kuwasaidia kupata vifaa hasa taulo na kuwaelekeza namna ya kutumia vifaa hivyo wakati wa hedhi .Tuhakikishe katika vikao vyetu mashuleni na katika mitaa yetu tunazungumaza suala la hedhi salama
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa