Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ametoamiezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), kufanyautafiti na sensa ya mamba katika Ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimayekuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwawananchi hususani wa jimbo la Songwe ikiwemo kuwavuna kama idadi yao itabainikakuwa kubwa.
Dk. Kigwangalla, ametoa agizo hilo jana katika kijiji chaMaleza kata ya Mbangala wilaya ya Songwe mkoani Songwe, alipokuwa akizungumzakwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwaajili ya kutatua mgogoro uliopo baina ya wananchi na Mamba wa Ziwa Rukwa.
“Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini yaWizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja na ndani ya miezi mitatu, wanipemajibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye ZiwaRukwa, wafanye sensa watuambie kuna Mamba wangapi lakini pia watushauri ninitufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababiaha athari kubwa kwenyemaisha ya watu wanaoishi jirani lakini pia wanaoutumia Ziwa.
“Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mambawameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, kwahivyo hata Mamba nao mwishowewataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndiomaana wameanza kutafuta binadamu anayekwenda Ziwani kwasababu sasa wanakuwa na njaa, inabidi wasogeeufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji” alifafanua Dk.Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamikombalimbali yaliyowasilishwa kwake na mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugoambaye amesema kumekuwepo na matukio mengi ya Mamba kushambulia na kuuwawananchi wa vijiji jirani wanaofata huduma mwambao wa Ziwa Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa